1 Waisraeli walikuwa kama mzabibu mzuri,mzabibu wenye kuzaa matunda.Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka,ndivyo walivyozidi kujijengea madhabahu.Kadiri nchi yao ilivyozidi kustawi,ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.
2 Mioyo yao imejaa udanganyifu.Sasa ni lazima wawajibike kwa hatia yao.Mwenyezi-Mungu atazibomoa madhabahu zaona kuziharibu nguzo zao.
3 Wakati huo watasema:“Hatuna tena mfalme,kwa kuwa hatumchi Mwenyezi-Mungu;lakini, naye mfalme atatufanyia nini?”
4 Wanachosema ni maneno matupu;wanaapa na kufanya mikataba ya bure;haki imekuwa si haki tena,inachipua kama magugu ya sumu shambani.