1 “Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda,Kutoka Misri nilimwita mwanangu.
2 Lakini kadiri nilivyozidi kuwaita,ndivyo walivyozidi kwenda mbali nami;waliendelea kuyatambikia Mabaali,na kuvifukizia ubani vinyago vya miungu.
3 Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea!Mimi mwenyewe niliwachukua mikononi mwangu;lakini hawakutambua kuwa mimi ndiye niliyewatunza.
4 Niliwaongoza kwa kamba za hurumanaam, kwa kamba za upendo;kama baba amwinuaye mtoto mpaka shavuni mwake,ndivyo nami nilivyokuwa kwao.Mimi niliinama chini na kuwalisha.