1 Basi, waiteni kaka zenu, “Watu wangu,” na dada zenu, “Waliohurumiwa.”
2 Mlaumuni mama yenu mlaumuni,maana sasa yeye si mke wanguwala mimi si mume wake.Mlaumuni aondokane na uasherati wake,ajiepushe na uzinzi wake.
3 La sivyo, nitamvua nguo abaki uchi,nitamfanya awe kama alivyozaliwa.Nitamfanya awe kama jangwa,nitamweka akauke kama nchi kavu.Nitamuua kwa kiu.
4 Na watoto wake sitawahurumia,maana ni watoto wa uzinzi.
5 Mama yao amefanya uzinzi,aliyewachukua mimba amefanya mambo ya aibu.Alisema; “Nitaambatana na wapenzi wangu,ambao hunipa chakula na maji,sufu na kitani, mafuta na divai.”
6 Basi, nitaiziba njia yake kwa miiba,nitamzungushia ukuta,asipate njia ya kutokea nje.
7 Atawafuata wapenzi wake,lakini hatawapata;naam, atawatafuta,lakini hatawaona.Hapo ndipo atakaposema,“Nitarudi kwa mume wangu wa kwanza;maana hapo kwanza nilikuwa nafuu kuliko sasa.”