5 Wewe utajikwaa mchana,naye nabii atajikwaa pamoja nawe usiku.Nitamwangamiza mama yako Israeli.
6 Watu wangu wameangamia kwa kutonijua,maana wewe kuhani umekataa mafundisho.Nimekukataa kuwa kuhani wangu.Kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako,nami pia nitawasahau watoto wako.
7 “Kadiri makuhani walivyoongezeka,ndivyo wote walivyozidi kuniasi.Basi, nitaigeuza fahari yao kuwa aibu.
8 Wanajishibisha kwa sadaka za watu wangu wenye dhambi.Wana hamu sana ya kuwaona wametenda dhambi.
9 Lakini yatakayowapata watu yatawapata makuhani;nitawaadhibu kwa sababu ya mwenendo wao,nitawalipiza matendo yao wenyewe.
10 Watakula, lakini hawatashiba;watazini, lakini hawatapata watoto,kwa sababu wameniacha mimi Mwenyezi-Mungu,na kufuata miungu mingine.
11 “Divai mpya na ya zamanihuondoa maarifa.