5 Kiburi cha Waisraeli chaonekana wazi;watu wa Efraimu watajikwaa katika hatia yao,nao watu wa Yuda watajikwaa pamoja nao.
6 Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng'ombe,kumtafuta Mwenyezi-Mungu;lakini hawataweza kumpata,kwa sababu amejitenga nao.
7 Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu,wamezaa watoto walio haramu.Mwezi mwandamo utawaangamiza,pamoja na mashamba yao.
8 “Pigeni baragumu huko Gibea,na tarumbeta huko Rama.Pigeni king'ora huko Beth-aveni.Enyi watu wa Benyamini, adui yenu yuko nyuma!
9 Siku nitakapotoa adhabuEfraimu itakuwa kama jangwa!Ninachotangaza miongoni mwa makabila ya Israeli,ni jambo litakalotukia kwa hakika.
10 Viongozi wa Yuda wamekuwawenye kubadili mipaka ya ardhi.Mimi nitawamwagia hasira yangu kama maji.
11 Efraimu ameteswa,haki zake zimetwaliwa;kwani alipania kufuata upuuzi.