7 Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu,wamezaa watoto walio haramu.Mwezi mwandamo utawaangamiza,pamoja na mashamba yao.
8 “Pigeni baragumu huko Gibea,na tarumbeta huko Rama.Pigeni king'ora huko Beth-aveni.Enyi watu wa Benyamini, adui yenu yuko nyuma!
9 Siku nitakapotoa adhabuEfraimu itakuwa kama jangwa!Ninachotangaza miongoni mwa makabila ya Israeli,ni jambo litakalotukia kwa hakika.
10 Viongozi wa Yuda wamekuwawenye kubadili mipaka ya ardhi.Mimi nitawamwagia hasira yangu kama maji.
11 Efraimu ameteswa,haki zake zimetwaliwa;kwani alipania kufuata upuuzi.
12 Hivyo mimi Mungu niko kama nondo kwa Efraimu,kama donda baya kwa watu wa Yuda.
13 Watu wa Efraimu walipogundua ugonjwa wao,naam, watu wa Yuda walipogundua donda lao,watu wa Efraimu walikwenda Ashurukuomba msaada kwa mfalme mkuu;lakini yeye hakuweza kuwatibu,hakuweza kuponya donda lenu.