3 Lakini Israeli amepuuza mambo mema,kwa hiyo, sasa adui watamfuatia.
4 “Walijiwekea wafalme bila kibali changu,walijiteulia viongozi ambao sikuwatambua.Wamejitengenezea miungu ya fedha na dhahabu,jambo ambalo litawaangamiza.
5 Watu wa Samaria, naichukia sanamu yenu ya ndama.Hasira yangu inawaka dhidi yenu.Mtaendelea mpaka lini kuwa na hatia?
6 Nanyi Waisraeli ni hivyohivyo!Na sanamu yenu hiyo fundi ndiye aliyeitengeneza.Yenyewe si Mungu hata kidogo.Naam! Sanamu ya ndama ya Samaria itavunjwavunjwa!
7 “Wanapanda upepo, watavuna kimbunga!Mimea yao ya nafaka iliyo mashambanihaitatoa nafaka yoyote.Na hata kama ikizaa,mazao yake yataliwa na wageni.
8 Waisraeli wamemezwa;sasa wamo kati ya mataifa mengine,kama chombo kisicho na faida yoyote;
9 kwa kuwa wamekwenda kuomba msaada Ashuru.Efraimu ni punda anayetangatanga peke yake;Efraimu amekodisha wapenzi wake.