8 Waisraeli wamemezwa;sasa wamo kati ya mataifa mengine,kama chombo kisicho na faida yoyote;
9 kwa kuwa wamekwenda kuomba msaada Ashuru.Efraimu ni punda anayetangatanga peke yake;Efraimu amekodisha wapenzi wake.
10 Wametafuta wapenzi kati ya watu wa mataifa,lakini mimi nitawakusanya mara.Na hapo watasikia uzito wa mzigo,ambao mfalme wa wakuu aliwatwika.
11 “Watu wa Efraimu wamejijengea madhabahu nyingi,na madhabahu hizo zimewazidishia dhambi.
12 Hata kama ningewaandikia sheria zangu mara nyingi,wao wangeziona kuwa kitu cha kigeni tu.
13 Wanapenda kutoa tambiko,na kula nyama yake;lakini mimi Mwenyezi-Mungu sipendezwi hata kidogo.Mimi nayakumbuka makosa yao;nitawaadhibu kwa dhambi zao;nitawarudisha utumwani Misri.
14 Waisraeli wamemsahau Muumba wao,wakajijengea majumba ya fahari;watu wa Yuda wamejiongezea miji ya ngome,lakini mimi nitaipelekea moto miji hiyo,na kuziteketeza ngome zao.”