1 Hapo, Mose pamoja na Waisraeli wakamwimbia Mwenyezi-Mungu wimbo huu,“Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu kwani ameshinda kwa fahari,farasi na mpandafarasi wake amewatosa baharini.
2 Mwenyezi-Mungu hunijalia nguvu na uwezo,yeye mwenyewe ndiye anayeniokoa.Yeye ni Mungu wangu nami nitamsifu,ni Mungu wa baba yangu nami nitamtukuza.
3 Mwenyezi-Mungu ni shujaa vitani;Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake.
4 “Magari na majeshi ya Farao ameyatumbukiza baharini,maofisa wake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.
5 Vilindi vya maji vimewafunika,wameporomoka baharini kama jiwe.