43 Hapo ndipo nitakapokutana na Waisraeli na utukufu wangu utapafanya pawe patakatifu.
44 Hema la mkutano na madhabahu nitavifanya vitakatifu; vilevile Aroni na wanawe nitawaweka wakfu ili wanitumikie kama makuhani.
45 Nitaishi kati ya Waisraeli, nami nitakuwa Mungu wao.
46 Hapo ndipo watakapotambua kuwa mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili niishi kati yao. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.