26 Kila mtu aliyehesabiwa tangu umri wa miaka ishirini na moja na zaidi alitoa mchango wake wa fedha gramu 5; na wanaume wote waliohesabiwa walikuwa 603,550.
27 Kilo 3,000 za fedha zilitumika kutengenezea vile vikalio 100 vya hema takatifu na lile pazia, yaani kilo 30 kwa kila kikalio.
28 Zile kilo 17 na gramu 75 zilizosalia, zilitumika kutengenezea kulabu za nguzo na kuvipaka vichwa vya nguzo na kuitengenezea vitanzi.
29 Jumla ya mchango wa shaba Waisraeli waliomtolea Mwenyezi-Mungu ilikuwa na uzito wa kilo 2124.
30 Bezaleli aliitumia shaba hiyo kutengenezea vikalio vya mlango wa hema la mkutano, madhabahu ya shaba pamoja na wavu wake wa shaba, vyombo vyote vya madhabahu,
31 vikalio vya ua uliolizunguka hema la mkutano na vya lango la ua, na vigingi vyote vya hema takatifu na vya ua.