12 Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
13 Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu.
14 Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka,
15 na ingae angani na kuiangazia dunia.” Ikawa hivyo.
16 Basi, Mungu akafanya mianga miwili mikubwa; ule mkubwa utawale mchana na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.
17 Mungu akaiweka mianga hiyo angani iiangazie dunia,
18 ipate kutawala mchana na usiku, na kuutenga mwanga na giza. Mungu akaona kuwa ni vyema.