7 Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena na kumzalia Yakobo mtoto wa pili wa kiume.
8 Hapo Raheli akasema, “Nimepigana miereka mikali na dada yangu, nami nimeshinda.” Kwa hiyo akamwita mtoto huyo Naftali.
9 Lea alipoona ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, na kumpa Yakobo ili awe mkewe.
10 Zilpa akamzalia Yakobo mtoto wa kiume.
11 Lea akasema, “Bahati njema.” Kwa hiyo akamwita mtoto huyo Gadi.
12 Zilpa, mtumishi wa Lea, alimzalia Yakobo mtoto wa pili wa kiume.
13 Lea akasema, “Bahati njema! Sasa wanawake wataniita heri.” Kwa hiyo akamwita mtoto huyo Asheri.