15 Aliposikia napiga kelele, aliliacha vazi lake, akakimbilia nje!”
16 Basi, yule mwanamke akaliweka vazi hilo mpaka mumewe aliporudi nyumbani.
17 Akamsimulia kisa kile akisema, “Huyu mtumishi Mwebrania uliyemleta kwetu alinijia ili kuniaibisha.
18 Lakini mara tu nilipopiga kelele, aliliacha vazi lake na kukimbilia nje.”
19 Basi, bwana wake Yosefu alipoyasikia maneno ya mkewe, kwamba ndivyo mtumishi wake alivyomtendea, akawaka hasira,
20 akamchukua Yosefu na kumtia gerezani, mahali walipofungwa wahalifu wa mfalme.
21 Lakini hata humo gerezani Mwenyezi-Mungu alikuwa pamoja na Yosefu akimfadhili hata kumfanya apendeke mbele ya mkuu wa gereza.