13 Noa alipokuwa na umri wa miaka 601, siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, maji yalikuwa yamekauka katika nchi. Noa akafunua kifuniko cha safina na alipotazama, akaona kwamba nchi ilikuwa imekauka.
14 Siku ya 27 ya mwezi wa pili, nchi ilikuwa imekauka kabisa.
15 Hapo, Mungu akamwambia Noa,
16 “Toka katika safina, wewe pamoja na mkeo, wanao na wake zao.
17 Toa pia viumbe wote hai wa kila aina waliokuwa pamoja nawe, ndege na wanyama na kila kiumbe kitambaacho, wapate kuzaa kwa wingi duniani, waongezeke na kuenea kila mahali duniani.”
18 Basi, Noa akatoka katika safina pamoja na wanawe na mkewe pamoja na wake za wanawe.
19 Wakatoka kufuatana na jamii zao, wanyama wote wa porini, viumbe wote watambaao, ndege wote na wanyama wote hai duniani.