1 Maana BWANA atamhurumia Yakobo, atamchagua Israeli tena, naye atawaweka katika nchi yao wenyewe; na mgeni atajiunga nao, nao wataambatana na nyumba ya Yakobo.
2 Na hao mataifa watawatwaa na kuwaleta mpaka mahali pao wenyewe, na nyumba ya Israeli watawamiliki, na kuwafanya watumishi na wajakazi katika nchi ya BWANA; nao watawachukua hali ya kufungwa watu wale waliowafunga wao, nao watawamiliki watu wale waliowaonea.
3 Tena itakuwa katika siku ile, ambayo BWANA atakupa raha baada ya huzuni yako, na baada ya taabu yako, na baada ya utumishi ule mgumu uliotumikishwa;
4 utatunga mithali hii juu ya mfalme wa Babeli, na kusema,Jinsi alivyokoma mwenye kuonea;Jinsi ulivyokoma mji ule wenye jeuri!
5 BWANA amelivunja gongo la wabaya,Fimbo ya enzi yao wenye kutawala.
6 Yeye aliyewapiga mataifa kwa ghadhabu,Kwa mapigo yasiyokoma;Aliyewatawala mataifa kwa hasira,Ameadhibiwa asizuie mtu.