4 Kwa ajili ya Yakobo, mtumishi wangu, na Israeli, mteule wangu, nimekuita kwa jina lako; nimekupa jina la sifa; ijapokuwa hukunijua.
5 Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua;
6 ili wapate kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.
7 Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.
8 Dondokeni, enyi mbingu, toka juu,Mawingu na yamwage haki;Nchi na ifunuke, ili kutoa wokovu,Nayo itoe haki ikamee pamoja;Mimi, BWANA, nimeiumba.
9 Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au kazi yako, Hana mikono?
10 Ole wake amwambiaye baba yake, Wazaa nini? Au mwanamke, Una utungu wa nini?