8 BWANA asema hivi, Wakati uliokubalika nimekujibu, na siku ya wokovu nimekusaidia; nami nitakuhifadhi, nitakutoa uwe agano la watu hawa, ili kuiinua nchi hii, na kuwarithisha urithi uliokuwa ukiwa;
9 kuwaambia waliofungwa, Haya, tokeni; na hao walio katika giza, Jionyesheni. Watajilisha katika njia, na juu ya majabali watapata malisho.
10 Hawataona njaa, wala hawataona kiu; hari haitawapiga, wala jua; kwa maana yeye aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza.
11 Nami nitafanya milima yangu yote kuwa njia, na njia kuu zangu zitatukuzwa zote.
12 Tazama, hawa watakuja kutoka mbali; na tazama, hawa kutoka kaskazini, na kutoka magharibi, na hawa kutoka nchi ya Sinimu.
13 Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi;Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima;Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake,Naye atawahurumia watu wake walioteswa.
14 Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau.