8 Maana nondo itawala kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na wokovu wangu hata vizazi vyote.
9 Amka, amka, jivike nguvu,Ee mkono wa Bwana;Amka kama katika siku zile za kale,Katika vizazi vile vya zamani.
10 Si wewe uliyemkata-kata Rahabu?Uliyemchoma yule joka?Si wewe uliyeikausha bahari,Na maji ya vilindi vikuu;Uliyevifanya vilindi kuwa njia,Ili wapite watu waliokombolewa?
11 Nao waliokombolewa na BWANA watarejea,Watafika Sayuni, wakiimba;Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao;Watapata shangwe na furaha;Huzuni na kuugua zitakimbia.
12 Mimi, naam, mimi, ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa kama majani?
13 Ukamsahau BWANA, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo afanyapo tayari kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye?
14 Yeye aliyehamishwa na kufungwa atafunguliwa kwa haraka; wala hatakufa na kushuka shimoni, wala chakula chake hakitapunguka.