3 Maana BWANA asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha.
4 Maana Bwana MUNGU asema hivi, Watu wangu hapo kwanza walishuka Misri ili wakae huko hali ya ugeni; na Mwashuri akawaonea bila sababu.
5 Basi sasa, nafanya nini hapa, asema BWANA, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema BWANA, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa.
6 Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.
7 Jinsi ilivyo mizuri juu ya milimaMiguu yake aletaye habari njema,Yeye aitangazaye amani,Aletaye habari njema ya mambo mema,Yeye autangazaye wokovu,Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!
8 Sauti ya walinzi wako!Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja;Maana wataona jicho kwa jicho,Jinsi BWANA arejeavyo Sayuni.
9 Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja,Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa;Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake,Ameukomboa Yerusalemu.