6 Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.
7 Jinsi ilivyo mizuri juu ya milimaMiguu yake aletaye habari njema,Yeye aitangazaye amani,Aletaye habari njema ya mambo mema,Yeye autangazaye wokovu,Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!
8 Sauti ya walinzi wako!Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja;Maana wataona jicho kwa jicho,Jinsi BWANA arejeavyo Sayuni.
9 Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja,Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa;Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake,Ameukomboa Yerusalemu.
10 BWANA ameweka wazi mkono wake mtakatifuMachoni pa mataifa yote;Na ncha zote za duniaZitauona wokovu wa Mungu wetu.
11 Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.
12 Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu BWANA atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde.