1 Haya, kila aonaye kiu, njoni majini,Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle;Naam, njoni, nunueni divai na maziwa,Bila fedha na bila thamani.
2 Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula?Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha?Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema,Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.
3 Tegeni masikio yenu, na kunijia;Sikieni, na nafsi zenu zitaishi;Nami nitafanya nanyi agano la milele,Naam, rehema za Daudi zilizo imara.
4 Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa kabila za watu.
5 Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.
6 Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,Mwiteni, maadamu yu karibu;