10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
12 Maana mtatoka kwa furaha,Mtaongozwa kwa amani;Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo;Na miti yote ya kondeni itapiga makofi.
13 Badala ya michongoma utamea msunobari,Na badala ya mibigili, mhadesi;Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina,Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.