2 Maana, tazama, giza litaifunika dunia,Na giza kuu litazifunika kabila za watu;Bali BWANA atakuzukia wewe,Na utukufu wake utaonekana juu yako.
3 Na mataifa wataijilia nuru yako,Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.
4 Inua macho yako, utazame pande zote;Wote wanakusanyana; wanakujia wewe;Wana wako watakuja kutoka mbali.Na binti zako watabebwa nyongani.
5 Ndipo utakapoona na kutiwa nuru,Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka;Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia,Utajiri wa mataifa utakuwasilia.
6 Wingi wa ngamia utakufunika,Ngamia vijana wa Midiani na Efa;Wote watakuja kutoka Sheba;Wataleta dhahabu na uvumba;Na kuzitangaza sifa za BWANA.
7 Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako,Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia;Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali,Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu.
8 Ni nani hawa warukao kama wingu,Na kama njiwa waendao madirishani kwao?