4 Kwa maana kabla mtoto huyo hajapata kujua kusema, Baba yangu, na Mama yangu, hazina za Dameski na mateka ya Samaria yatachukuliwa mbele ya mfalme wa Ashuru.
5 Kisha BWANA akasema nami mara ya pili, akaniambia,
6 Kwa sababu watu hawa wameyakataa maji ya Shiloa yapitayo polepole, na kufurahi kwa ajili ya Resini na huyo mwana wa Remalia,
7 basi sasa angalia; Bwana aleta juu yao maji ya huo Mto, yenye nguvu, mengi sana, nayo ni mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; naye atakuja, na kupita juu ya mifereji yake yote, atafurika juu ya kingo zake zote;
8 naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.
9 Fanyeni ghasia, enyi kabila za watu,Nanyi mtavunjwa vipande vipande;Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali;Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande;Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande.
10 Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika;Semeni neno, lakini halitasimama;Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.