10 Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi,Wewe usikubali.
11 Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi,Na tuvizie ili kumwaga damu;Tumwotee asiye na hatia, bila sababu;
12 Tuwameze hai kama kuzimu,Na wazima, kama wao washukao shimoni.
13 Tutapata mali yote ya thamani,Tutazijaza nyumba zetu mateka.
14 Wewe utashirikiana nasi;Tutakuwa na vitu vyote shirika.
15 Mwanangu, usiende njiani pamoja nao;Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.
16 Maana miguu yao huenda mbio maovuni,Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.