Mit. 10 SUV

Mithali za Sulemani.

KITABU CHA PILI

1 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye;Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.

2 Hazina za uovu hazifaidii kitu;Bali haki huokoa na mauti.

3 BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa;Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.

4 Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini;Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.

5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima;Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.

6 Baraka humkalia mwenye haki kichwani;Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu.

7 Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka;Bali jina la mtu mwovu litaoza.

8 Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo;Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.

9 Aendaye kwa unyofu huenda salama;Bali apotoshaye njia zake atajulikana.

10 Akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko;Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.

11 Kinywa chake mwenye haki ni chemchemi ya uzima;Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu,

12 Kuchukiana huondokesha fitina;Bali kupendana husitiri makosa yote.

13 Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu;Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu.

14 Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa;Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.

15 Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu;Uangamivu wa maskini ni umaskini wao.

16 Kazi yake mwenye haki huuelekea uzima;Mazao ya wabaya huuelekea dhambi.

17 Akubaliye kurudiwa huwa katika njia ya uzima;Bali yeye aachaye maonyo hukosa.

18 Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo,Na yeye asingiziaye ni mpumbavu.

19 Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu;Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.

20 Ulimi wa mwenye haki ni kama fedha teule;Moyo wa mtu mbaya haufai kitu.

21 Midomo ya mwenye haki hulisha watu wengi;Bali wapumbavu hufa kwa kuwa hawana ufahamu.

22 Baraka ya BWANA hutajirisha,Wala hachanganyi huzuni nayo.

23 Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo;Bali mtu mwenye ufahamu ana hekima.

24 Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia;Na wenye haki watapewa matakwa yao.

25 Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena;Bali mwenye haki ni msingi wa milele.

26 Kama siki menoni, na kama moshi machoni,Ndivyo alivyo mtu mvivu kwao wamtumao.

27 Kumcha BWANA kwaongeza siku za mtu;Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa.

28 Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha;Bali kutaraji kwao wasio haki kutapotea.

29 Njia ya BWANA ni kimbilio lake mtu mkamilifu;Bali ni uharibifu kwao watendao maovu.

30 Mwenye haki hataondolewa milele;Bali wasio haki hawatakaa katika nchi.

31 Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima;Bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali.

Sura

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31