Mit. 13 SUV

1 Mwana mwenye hekima husikiliza mausia ya babaye;Bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.

2 Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake;Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri.

3 Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake;Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.

4 Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu;Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.

5 Mwenye haki huchukia kusema uongo;Bali mtu mbaya huwa karaha, hupatwa na aibu.

6 Haki humlinda yeye aliye mnyofu katika njia yake;Bali ubaya humwangusha mwenye dhambi.

7 Kuna mtu mwenye kujitajirisha, lakini hana kitu;Kuna ajifanyaye kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.

8 Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake;Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote.

9 Nuru ya mwenye haki yang’aa sana;Bali taa ya mtu mbaya itazimika.

10 Kiburi huleta mashindano tu;Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.

11 Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka;Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.

12 Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua.Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.

13 Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu;Bali yeye aiogopaye amri atapewa thawabu.

14 Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima,Ili kuepukana na tanzi za mauti.

15 Ufahamu mwema huleta upendeleo;Bali njia ya haini huparuza.

16 Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa;Bali mpumbavu hueneza upumbavu.

17 Mjumbe mbaya huanguka maovuni;Bali mjumbe mwaminifu ni afya.

18 Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa;Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa.

19 Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu;Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.

20 Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima;Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.

21 Uovu huwaandamia wenye dhambi;Bali mwenye haki atalipwa mema.

22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi;Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.

23 Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini;Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma.

24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe;Bali yeye ampendaye humrudi mapema.

Sura

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31