Mit. 21 SUV

1 Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA;Kama mifereji ya maji huugeuza po pote apendapo.

2 Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe;Bali BWANA huipima mioyo.

3 Kutenda haki na hukumuHumpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.

4 Macho yenye kiburi, na moyo wa kutakabari,Hata ukulima wa waovu, ni dhambi.

5 Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu;Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.

6 Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongoNi moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti.

7 Jeuri ya wabaya itawaondolea mbali;Kwa sababu wamekataa kutenda hukumu.

8 Njia yake aliyelemewa na dhambi imepotoka sana;Bali mtu aliye safi, kazi yake ni sawasawa.

9 Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini,Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.

10 Nafsi ya mtu mbaya hutamani uovu;Jirani yake hapati fadhili machoni pake.

11 Mwenye mzaha aadhibiwapo, mjinga hupata hekima;Na mwenye hekima afundishwapo, hupokea maarifa.

12 Mwenye haki huitafakari nyumba ya mtu mbaya;Jinsi wabaya waangushwavyo wakaangamia.

13 Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini,Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa.

14 Kipawa cha siri hutuliza hasira;Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali.

15 Ni furaha yao wenye haki kutenda hukumu;Lakini ni uharibifu kwao watendao maovu.

16 Mtu aikosaye njia ya busaraAtakaa katika mkutano wao waliokufa.

17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini;Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri.

18 Mtu asiye haki ni fidia ya wenye haki;Naye afanyaye hila ni badala ya watu wa adili.

19 Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika;Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.

20 Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima;Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.

21 Aandamaye haki na fadhili,Ataona uhai na haki na heshima.

22 Mwenye hekima huupandia mji wao wenye nguvu;Na kuziangusha nguvu za tumaini lao.

23 Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake,Atajilinda nafsi yake na taabu.

24 Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi;Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.

25 Matakwa yake mtu mvivu humfisha,Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi.

26 Kuna atamaniye kwa choyo mchana kutwa;Bali mwenye haki hutoa wala hanyimi.

27 Sadaka ya wasio haki ni chukizo;Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya!

28 Shahidi wa uongo atapotea;Bali mtu asikiaye atasema maneno yadumuyo.

29 Asiye haki huufanya uso wake kuwa mgumu;Bali mtu mnyofu huzifikiri njia zake.

30 Hapana hekima, wala ufahamu,Wala shauri, juu ya BWANA.

Sura

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31