Mit. 11 SUV

1 Mizani ya hadaa ni chukizo kwa BWANA;Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.

2 Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu;Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.

3 Ukamilifu wao wenye haki utawaongozaBali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.

4 Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu;Bali haki huokoa na mauti.

5 Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake;Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake.

6 Haki yao wenye haki itawaokoa;Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.

7 Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea;Na matumaini ya uovu huangamia.

8 Mwenye haki huokolewa katika dhiki,Na mtu mwovu ataiingia badala yake.

9 Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake;Bali wenye haki watapona kwa maarifa.

10 Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi;Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele.

11 Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki;Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.

12 Asiye na akili humdharau mwenziwe;Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.

13 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri;Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.

14 Pasipo mashauri taifa huanguka;Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.

15 Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;Achukiaye mambo ya dhamana yu salama.

16 Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima;Na watu wakali hushika mali siku zote.

17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake;Aliye mkali hujisumbua mwili wake.

18 Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu;Apandaye haki ana thawabu ya hakika.

19 Haki huelekea uzima;Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe.

20 Wenye kuhalifu moyoni ni chukizo kwa BWANA;Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza.

21 Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu;Bali wazao wa wenye haki wataokoka.

22 Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe,Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili.

23 Haja ya mwenye haki ni mema tu;Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu.

24 Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi;Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.

25 Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa;Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.

26 Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani;Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake.

27 Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili;Atafutaye madhara, hayo yatamjia.

28 Azitegemeaye mali zake ataanguka;Mwenye haki atasitawi kama jani.

29 Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo;Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili.

30 Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima;Na mwenye hekima huvuta roho za watu.

Sura

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31