11 Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi,Na tuvizie ili kumwaga damu;Tumwotee asiye na hatia, bila sababu;
12 Tuwameze hai kama kuzimu,Na wazima, kama wao washukao shimoni.
13 Tutapata mali yote ya thamani,Tutazijaza nyumba zetu mateka.
14 Wewe utashirikiana nasi;Tutakuwa na vitu vyote shirika.
15 Mwanangu, usiende njiani pamoja nao;Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.
16 Maana miguu yao huenda mbio maovuni,Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.
17 Kwa kuwa mtego hutegwa bure,Mbele ya macho ya ndege ye yote.