23 Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu;Tazama, nitawamwagia roho yangu,Na kuwajulisheni maneno yangu.
24 Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa;Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;
25 Bali mmebatilisha shauri langu,Wala hamkutaka maonyo yangu;
26 Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu,Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;
27 Hofu yenu ifikapo kama tufani,Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli,Dhiki na taabu zitakapowafikia.
28 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika;Watanitafuta kwa bidii, wasinione.
29 Kwa kuwa walichukia maarifa,Wala hawakuchagua kumcha BWANA.