7 Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako,Wala usiiache sheria ya mama yako,
9 Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako,Na mikufu shingoni mwako.
10 Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi,Wewe usikubali.
11 Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi,Na tuvizie ili kumwaga damu;Tumwotee asiye na hatia, bila sababu;
12 Tuwameze hai kama kuzimu,Na wazima, kama wao washukao shimoni.
13 Tutapata mali yote ya thamani,Tutazijaza nyumba zetu mateka.