1 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye;Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.
2 Hazina za uovu hazifaidii kitu;Bali haki huokoa na mauti.
3 BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa;Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.
4 Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini;Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima;Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
6 Baraka humkalia mwenye haki kichwani;Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu.
7 Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka;Bali jina la mtu mwovu litaoza.