14 Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa;Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.
15 Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu;Uangamivu wa maskini ni umaskini wao.
16 Kazi yake mwenye haki huuelekea uzima;Mazao ya wabaya huuelekea dhambi.
17 Akubaliye kurudiwa huwa katika njia ya uzima;Bali yeye aachaye maonyo hukosa.
18 Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo,Na yeye asingiziaye ni mpumbavu.
19 Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu;Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.
20 Ulimi wa mwenye haki ni kama fedha teule;Moyo wa mtu mbaya haufai kitu.