20 Ulimi wa mwenye haki ni kama fedha teule;Moyo wa mtu mbaya haufai kitu.
21 Midomo ya mwenye haki hulisha watu wengi;Bali wapumbavu hufa kwa kuwa hawana ufahamu.
22 Baraka ya BWANA hutajirisha,Wala hachanganyi huzuni nayo.
23 Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo;Bali mtu mwenye ufahamu ana hekima.
24 Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia;Na wenye haki watapewa matakwa yao.
25 Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena;Bali mwenye haki ni msingi wa milele.
26 Kama siki menoni, na kama moshi machoni,Ndivyo alivyo mtu mvivu kwao wamtumao.