24 Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia;Na wenye haki watapewa matakwa yao.
25 Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena;Bali mwenye haki ni msingi wa milele.
26 Kama siki menoni, na kama moshi machoni,Ndivyo alivyo mtu mvivu kwao wamtumao.
27 Kumcha BWANA kwaongeza siku za mtu;Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa.
28 Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha;Bali kutaraji kwao wasio haki kutapotea.
29 Njia ya BWANA ni kimbilio lake mtu mkamilifu;Bali ni uharibifu kwao watendao maovu.
30 Mwenye haki hataondolewa milele;Bali wasio haki hawatakaa katika nchi.