3 BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa;Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.
4 Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini;Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima;Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
6 Baraka humkalia mwenye haki kichwani;Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu.
7 Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka;Bali jina la mtu mwovu litaoza.
8 Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo;Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.
9 Aendaye kwa unyofu huenda salama;Bali apotoshaye njia zake atajulikana.