11 Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki;Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.
12 Asiye na akili humdharau mwenziwe;Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
13 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri;Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.
14 Pasipo mashauri taifa huanguka;Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.
15 Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;Achukiaye mambo ya dhamana yu salama.
16 Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima;Na watu wakali hushika mali siku zote.
17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake;Aliye mkali hujisumbua mwili wake.