24 Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi;Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.
25 Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa;Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.
26 Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani;Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake.
27 Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili;Atafutaye madhara, hayo yatamjia.
28 Azitegemeaye mali zake ataanguka;Mwenye haki atasitawi kama jani.
29 Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo;Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili.
30 Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima;Na mwenye hekima huvuta roho za watu.