5 Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake;Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake.
6 Haki yao wenye haki itawaokoa;Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.
7 Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea;Na matumaini ya uovu huangamia.
8 Mwenye haki huokolewa katika dhiki,Na mtu mwovu ataiingia badala yake.
9 Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake;Bali wenye haki watapona kwa maarifa.
10 Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi;Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele.
11 Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki;Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.