8 Mwenye haki huokolewa katika dhiki,Na mtu mwovu ataiingia badala yake.
9 Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake;Bali wenye haki watapona kwa maarifa.
10 Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi;Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele.
11 Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki;Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.
12 Asiye na akili humdharau mwenziwe;Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
13 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri;Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.
14 Pasipo mashauri taifa huanguka;Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.