4 Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu;Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.
5 Mwenye haki huchukia kusema uongo;Bali mtu mbaya huwa karaha, hupatwa na aibu.
6 Haki humlinda yeye aliye mnyofu katika njia yake;Bali ubaya humwangusha mwenye dhambi.
7 Kuna mtu mwenye kujitajirisha, lakini hana kitu;Kuna ajifanyaye kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.
8 Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake;Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote.
9 Nuru ya mwenye haki yang’aa sana;Bali taa ya mtu mbaya itazimika.
10 Kiburi huleta mashindano tu;Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.