21 Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara;Utamu wa maneno huongeza elimu.
22 Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao;Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao.
23 Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake;Huzidisha elimu ya midomo yake.
24 Maneno yapendezayo ni kama sega la asali;Ni tamu nafsini, na afya mifupani.
25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu;Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
26 Nafsi yake mfanya kazi hujifanyia kazi;Maana kinywa chake humtia bidii.
27 Mtu asiyefaa kitu huchimba shimo la madhara;Katika midomo yake mna moto uteketezao.