3 Mkabidhi BWANA kazi zako,Na mawazo yako yatathibitika.
4 BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake;Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.
5 Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA;Hakika, hatakosa adhabu.
6 Kwa rehema na kweli uovu husafishwa;Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu.
7 Njia za mtu zikimpendeza BWANA,Hata adui zake huwapatanisha naye.
8 Afadhali mali kidogo pamoja na haki,Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake;Bali BWANA huziongoza hatua zake.