9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake;Bali BWANA huziongoza hatua zake.
10 Kukata maneno huwa katika midomo ya mfalme;Kinywa chake hakitakosa katika hukumu.
11 Mizani ya haki na vitanga vyake ni vya BWANA;Mawe yote ya mfukoni ni kazi yake.
12 Wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo;Maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki.
13 Midomo ya haki ni furaha ya wafalme;Nao humpenda yeye asemaye yaliyo sawa.
14 Hasira ya mfalme ni kama wajumbe wa mauti;Lakini mtu mwenye hekima ataituliza.
15 Kuna uhai katika nuru ya uso wa mfalme,Na fadhili zake ni kama wingu la masika.