14 Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji;Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.
15 Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki;naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki;Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.
16 Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima,Ikiwa hana moyo wa ufahamu?
17 Rafiki hupenda sikuzote;Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.
18 Aliyepungukiwa na akili hupana mkono na mtu;Na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake.
19 Apendaye ugomvi hupenda dhambi;Auinuaye sana mlango wake hutafuta uharibifu.
20 Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema;Na mwenye ulimi wa upotofu huanguka katika misiba.