2 Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu;Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.
3 Kalibuni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu;Bali BWANA huijaribu mioyo.
4 Mtenda mabaya husikiliza midomo ya uovu;Na mwongo hutega sikio lake kusikiliza ulimi wa madhara.
5 Amdhihakiye maskini humsuta Muumba wake;Naye aufurahiaye msiba hatakosa adhabu.
6 Wana wa wana ndio taji ya wazee,Na utukufu wa watoto ni baba zao.
7 Maneno mazuri hayapendezi kinywani mwa mpumbavu;Siuze midomo ya uongo kinywani mwa mkuu.
8 Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho;Kila kigeukapo hufanikiwa.