21 Azaaye mpumbavu ni kwa huzuni yake mwenyewe;Wala baba wa mpumbavu hana furaha.
22 Moyo uliochangamka ni dawa nzuri;Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.
23 Asiye haki hutoa rushwa kifuani,Ili kuzipotosha njia za hukumu.
24 Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu;Bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia.
25 Mwana mpumbavu ni huzuni kwa babaye,Na uchungu kwa mamaye aliyemzaa.
26 Tena kumwadhibu mwenye haki si vizuri;Wala si kwema kuwapiga wakuu kwa unyofu wao.
27 Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa;Na mwenye roho ya utulivu ana busara.