7 Maneno mazuri hayapendezi kinywani mwa mpumbavu;Siuze midomo ya uongo kinywani mwa mkuu.
8 Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho;Kila kigeukapo hufanikiwa.
9 Afunikaye kosa hutafuta kupendwa;Bali yeye akashifuye neno hutenga rafiki.
10 Lawama hupenya moyoni mwa mwenye ufahamu,Kuliko mapigo mia moyoni mwa mpumbavu.
11 Mtu mwovu hataki neno ila kuasi tu;Kwa hiyo mjumbe mkali atatumwa kwake.
12 Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake,Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake.
13 Yeye arudishaye mabaya badala ya mema,Mabaya hayataondoka nyumbani mwake.